Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara

Matukio katika picha

Tazama Ujumbe wa Kamishna Jenerali

Jeshi la Zimamoto lipo tayari Saa 24

Piga Namba ya Dharura 114, tuje tuhudumie.

Huduma Zinazotolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Jukumu la Jeshi kutoa huduma ya maokozi  nchi kavu, majini na angani. Jukumu hili hutekelezwa kwa njia tofauti ikiwemo kuandaa mikakati ya maokozi iwapo dharura itatokea kwa kusudi la kupunguza idadi ya vifo pindi yatokeapo mafuriko, ajali za barabarani, tetemeko la ardhi. Kutoa ushauri kwa Serikali pamoja na Mashirika binafsi juu ya huduma ya maokozi. Huduma hizo hutoolewa pia bandari pamoja na viwanja vya ndege.

Ni jukumu la Jeshi kutoa huduma ya usalama kwa jamii husika katika shughuli mbalimbali kama vile Matamasha, Michezo, sherehe za mahafali na katika mashindano ya magari/ mbio za magari ‘car sport rally’. Katika shughuli hii Jeshi hutilia mkazo kwa kuweka gari la kuzimia moto na Maokozi pamoja na Askari ikiwemo kuandaa mikakati ya maokozi iwapo dharura itatokea kwa kusudi la kupunguza idadi ya vifo pindi majanga yanapotokea katika mazingira hayo.

Huduma hizo hutoolewa pia bandari pamoja na viwanja vya ndege.

Jeshi la zimamoto na uokaoji linajukumu la kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto kwa mujibu wa Sheria na kanuni za ukaguzi na vyeti.ukaguzi huo huenda sanjari na ukusanyajiwa maduhuli ya serikali.makusanyo hayo huingia moja kwa moja Hazina katika mfuko mkuu wa Serikali amabpo Jeshi hurejeshewa  49 % ya makusanyo hayo.

Jukumu la jeshi ni kutoa huduma za uzimamji moto katika maeneo mbalimbali . kuandaa mipango mikakati ya uzimaji moto , kukagua vifaa mbalimbali na kuhakiki umadhubuti wake kabla ya kuingizwa nchini, pamoja na kufanya uchunguzi wa mioto ya hujuma.

Jeshi linajukumu la kufanya uchunguzi dhidi ya vyanzo mbalimbali zisababishi hatarishi vya moto pamoja na kuchukua tahadhari.Hivyo Jeshi huanda na kutekeleza mipango mikakati pamoja na kufanya tathimini ya majanga yatokenayo na moto. Kuandaa mipango ya ukaguzi wa majengo,mtambo ya gesi, viwanda  na maeneo mbalimbali hatarishi.

Idara hutoa  elimu ya kinga na tahadhari ya moto , na kutoa habari na taarifa mbalimbali ya juu ya usalama wa moto pamoja na huduma za zimamoto. Katika utoaji wa elimu pia Jeshi hutoa ushauri wa utoaji na upatikanaji wa huduma za Zimamoto na maokozi.

Pia jeshi lina jukumu la kupitia michoro yote ya majengo marefu na mafupi kwa lengo la kutoa maelekezo na ushauri kuhusu vifaa vya kinga na tahadhari ya moto pamoja na usalama wa watumiaji wa jengo husika kuhusiana na majanga mbalimbali yanayoweza kutokea katika jamii husika.

Jeshi lina jukumu la kutoa mafunzo jinsi ya kukabiliana na majanga ya moto ili kuepusha vifo vya watu wengi na pia kuokoa mali za watu. Mafunzo hayo hutolewa kwenye vyombo vya habari na pia sehemu zenye mkusanyiko wa watu wengi kama kwenye vituo vya mabasi, shuleni na taasisi mbalimbali. Mafunzo yanatolewa kuhusiana na jinsi ya kutumia vizimiamoto vya huduma ya kwanza na aina gani ya kizimiamoto unatakiwa utumie kutokana na aina ya moto.

Jeshi hushiriki katika shughuli za upangaji miji ili kupunguza uwezekano wa kutokea majanga mbalimbali katika makazi, na pia kusaidia njia rahisi za kufika katika matukio ya moto, ‘ambulance’ na huduma zingine ili kuokoa maisha na mali, pia Jeshi lina jukumu la kushiriki katika hatua za awali za upangaji wa miji kwa kuzingatia kanuni za usalama ili kupunguza athari pindi janga linapotokea.

Shuhuda mbalimbali kutoka kwa jamii


Nachukua fursa hii kulishukuru Jeshi la Zima moto na uokaji kuweza kuzima moto ulikokuwa ukiendelea katika shulke yetu,Walifanikiwa kudhiti moto huo kwa ufanisi mkubwa.Mungu ibariki Iyunga sekondari na ibariki Tanzania
Iyunga High School
Mkuu wa shule
Nalipongeza na kulisifu jeshi la zimamoto na uokaji katika uzalendo na juhudi ya kufanya kazi na kufanikiwa kuzima moto uliokuwa ukiendelea katika shule yetu
Mtwara Tech
Mkuu wa shule
Kwa keweli nimeshuhuidia umakini wa jeshi nla zima moto na uokoji katioka juhudi zake za kuzima moto katika soko letu lka sido hapa jijini Mbeya.Hongerini  kwa kazi nzuri
Soko la sido
Mfanyabiashara

Tunaomba ushiriki nasi Kuokoa Maisha ya Watu na Mali

Habari Mpya

Takwimu Zetu za Mwaka 2017/2018

Baadhi ya Takwimu za Mwaka 2016,Jinsi lilivyo shiriki kutoa huduma kwa wananchi wa Tanzania Bara

Majengo yaliokolewa
Mali zingine zilizookolewa
Simu Zilizopokelewa
Simu zilizofanyiwa kazi
Watu Walio okolewa

Wadau Wetu