Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara

Zifuatazo ni huduma zinazotolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

UTOAJI WA ELIMU KWA UMMA

Idara hutoa  elimu ya kinga na tahadhari ya moto , na kutoa habari na taarifa mbalimbali ya juu ya usalama wa moto pamoja na huduma za zimamoto. Katika utoaji wa elimu pia Jeshi hutoa ushauri wa utoaji na upatikanaji wa huduma za Zimamoto na maokozi.Idara hutoa  elimu ya kinga na tahadhari ya moto , na kutoa habari na taarifa mbalimbali ya juu ya usalama wa moto pamoja na huduma za zimamoto. Katika utoaji wa elimu pia Jeshi hutoa ushauri wa utoaji na upatikanaji wa huduma za Zimamoto na maokozi.

UCHUNGUZI NA TAHADHARI DHIDI YA MAJANGA YA MOTO

Jeshi linajukumu la kufanya uchunguzi dhidi ya vyanzo mbalimbali zisababishi hatarishi vya moto pamoja na kuchukua tahadhari.Hivyo Jeshi huanda na kutekeleza mipango mikakati pamoja na kufanya tathimini ya majanga yatokenayo na moto. Kuandaa mipango ya ukaguzi wa majengo,mtambo ya gesi, viwanda  na maeneo mbalimbali hatarishi.

STAND BY

Ni jukumu la Jeshi kutoa huduma ya usalama kwa jamii husika katika shughuli mbalimbali kama vile Matamasha, Michezo, sherehe za mahafali na katika mashindano ya magari/ mbio za magari ‘car sport rally’. Katika shughuli hii Jeshi hutilia mkazo kwa kuweka gari la kuzimia moto na Maokozi pamoja na Askari ikiwemo kuandaa mikakati ya maokozi iwapo dharura itatokea kwa kusudi la kupunguza idadi ya vifo pindi majanga yanapotokea katika mazingira hayo.

UKAGUZI NA UKUSANYAJI WA MADUHULI YA SERIKALI

Jeshi la zimamoto na uokaoji linajukumu la kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto kwa mujibu wa Sheria na kanuni za ukaguzi na vyeti.ukaguzi huo huenda sanjari na ukusanyajiwa maduhuli ya serikali.makusanyo hayo huingia moja kwa moja Hazina katika mfuko mkuu wa Serikali amabpo Jeshi hurejeshewa  49 % ya makusanyo hayo.

KUSOMA RAMANI ZA MAJENGO NA KUTOA USHAURI

Pia jeshi lina jukumu la kupitia michoro yote ya majengo marefu na mafupi kwa lengo la kutoa maelekezo na ushauri kuhusu vifaa vya kinga na tahadhari ya moto pamoja na usalama wa watumiaji wa jengo husika kuhusiana na majanga mbalimbali yanayoweza kutokea katika jamii husika.

KUTOA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA MAJANGA YA MOTO

Jeshi lina jukumu la kutoa mafunzo jinsi ya kukabiliana na majanga ya moto ili kuepusha vifo vya watu wengi na pia kuokoa mali za watu. Mafunzo hayo hutolewa kwenye vyombo vya habari na pia sehemu zenye mkusanyiko wa watu wengi kama kwenye vituo vya mabasi, shuleni na taasisi mbalimbali. Mafunzo yanatolewa kuhusiana na jinsi ya kutumia vizimiamoto vya huduma ya kwanza na aina gani ya kizimiamoto unatakiwa utumie kutokana na aina ya moto.

KUSHIRIKI KATIKA MPANGO WA UPANGAJI WA MIJI, HALMASHAURI, MIJI MIDOGO NA VIJIJI.

Jeshi hushiriki katika shughuli za upangaji miji ili kupunguza uwezekano wa kutokea majanga mbalimbali katika makazi, na pia kusaidia njia rahisi za kufika katika matukio ya moto, ‘ambulance’ na huduma zingine ili kuokoa maisha na mali, pia Jeshi lina jukumu la kushiriki katika hatua za awali za upangaji wa miji kwa kuzingatia kanuni za usalama ili kupunguza athari pindi janga linapotokea.

MAOKOZI

Jukumu la Jeshi kutoa huduma ya maokozi  nchi kavu, majini na angani. Jukumu hili hutekelezwa kwa njia tofauti ikiwemo kuandaa mikakati ya maokozi iwapo dharura itatokea kwa kusudi la kupunguza idadi ya vifo pindi itokeapo mafuriko, ajali za barabarani,tetemeko la ardhi.,kutoa ushauri kwa serikali pamoja na mashirika binafsi juu ya huduma ya maokozi. Huduma hizo hutoolewa pia bandari pamoja na viwanja vya ndege.

HUDUMA ZA UZIMAJI MOTO ‘FIRE OPERATIONAL SERVICE’

Jukumu la jeshi ni kutoa huduma za uzimamji moto katika maeneo mbalimbali . kuandaa mipango mikakati ya uzimaji moto , kukagua vifaa mbalimbali na kuhakiki umadhubuti wake kabla ya kuingizwa nchini, pamoja na kufanya uchunguzi wa mioto ya hujuma.