Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara

Uncategorized

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini – Thobias Andengenye anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna Mstaafu wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CF (OPS) Rogatius Peter Kipali, kilichotokea mapema leo Semptemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake Mombasa, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anatoa pole kwa Maafisa, Askari na Watumishi wote wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, familia ya Marehemu na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna tofauti tofauti.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na familia ya Marehemu linaendelea kuratibu shughuli za msiba huo na taarifa za Mazishi zitatolewa baadaye baada ya taratibu zote kukamilika.

 

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi

Amina.

 

 IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

 

Watu wengi wamekuwa wakikuta na kuvipita vifaa mithili ya mabomba ya kutoa maji pembezoni mwa barabara, maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu, viwanja vya ndege au viwanja vya michezo bila kufahamu vinafanya kazi gani.

Wengine hudhani ni mapambo ya barabara au alama Fulani kwenye maeneo hayo, ambapo baadhi yao hudiriki kuyatumia kinyume na kazi yake kutokana na kutotambua matumizi yake.

Mabomba haya (fire hydrants) sio mapambo bali ni mfumo uliounganishwa na mabomba makubwa ya maji, na kuwa visima vya maji ambapo gari la Zimamoto huchukua maji. Visima hivi vimejengwa makusudi kwa ajili ya kulirahisishia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea.

Mabomba hayo (Fire Hydrant) yana msukumo mkubwa wa maji na kusababisha maji yatoke kwa wingi na kwamuda mfupi. Uwepo wa vifaa hivyo sehemu mbalimbali za makazi ya watu na maeneo mengineyo hurahisisha zoezi zima la uzimaji moto, kwani pindi gari la kuzima moto linapoishiwa maji hujazwa hapohapo badala ya kuyafuata mbali na eneo la tukio.

Kwa kawaida magari ya zimamoto yana ujazo tofauti wa maji kuanzia lita 2000 hadi lita 16,000 ambapo ni ujazo mkubwa zaidi. Magari haya hubeba maji ya awali kwa ajili ya huduma ya kwanza ndio maana visima hivyo ni muhimu kuwepo.

Kwa nini tunasema ni maji kwa ajili ya huduma ya kwanza, ni kwa sababu ujazo wa maji yanayobebwa na gari la zimamoto ambao ni kati ya lita 2000 na lita 16000, hutoka kwamsukumo mkubwa, ambao kwa dakika moja maji yatatoka zaidi ya lita 1000 ukiwa unatumia mstari mmoja wa mpira wa maji (hose) na kusababisha maji hayo kuisha kwa muda mfupi.

Ukosefu wa visima hivyo sehemu mbalimbali, unapelekea Jeshi kushindwa kukabiliana na majanga ya moto kwa ufanisi baada ya maji yanayokuwa kwenye gari kuisha na kuwalazimu kwenda eneo la mbali.

Ingawa Jeshi la zimamoto na uokoaji linajitahidi kadri iwezekanavyo kuhakikisha linakabiliana vya kutosha na majanga ya moto kwa kusambaza visima hivi vya maji, lakini marakadhaa limekuwa linakumbana na changamoto mbalimbali hasa miundombinu.

Katika kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa, tayari baadhi ya Mikoa kama vile Dar es Salaam, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha na Tanga imejitahidi kuhakikisha miundombinu yake inakidhi kuruhusu ujenzi wa visima vya maji ya kuzimia moto na utaratibu umeandaliwa kuhakikisha mikoa Mingine inaboresha miundombinu yake kwa kuzingatia ujenzi wa huduma hiyo.

Pamoja na changamoto hizo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji bado linatekeleza wajibu wake kwa kuwa elimisha wananchi namna ya kutunza miundombinu hiyo na kusambaza mifumo hiyo kwa kiwango kinacho hitajika.

Wito kwa wananchi tuyatunze mabomba hayo (fire hydrant) kutokana na kuwa na umuhimu katika kurahisisha shughuli za kupambana na majanga ya moto, kwani kumekuwa na wimbi kubwa la uuzaji wa vyuma chakavu.

 

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimkabidhi zawadi Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko, kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, katika Tamasha la Usalama barabarani lilofanyika katika Viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam, (Kulia) Rais Mstaafu wa Awamu Pili Ali Hassan Mwinyi, (Wapili Kulia) Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko.

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Emmanuel Kibona (Katikati) akimpa maelekezo mmoja wa washiriki, ya namba ya dharura ya Jeshi hilo 114 inayotumiwa na wananchi kutoa taarifa pindi wanapopatwa na majanga ya moto, wakati wa Tamasha la Usalama barabarani lilofanyika katika Viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam.

Timu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na timu ya Jeshi la Polisi, wakiwa tayari kwa mpambano wa uvutaji Kamba katika kusheheresha Tamasha la Usalama barabarani, lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimvisha cheo Kamishna wa Divisheni ya Operesheni Billy Mwakatage, wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimvisha cheo Kamishna wa Divisheni ya Usalama dhidi ya Moto, Jesuald Ikonko wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimsikiliza Msemaji wa Jeshi hilo Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi, akitoa utambulisho mfupi wa Makamishna wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Kamishna wa Divisheni ya Oparesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, akila kiapo cha Utii mbele ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Kamishna wa Divisheni ya Usalama dhidi ya Moto wa Jeshi la Zimamoto na, Jesuald Ikonko, akila kiapo cha Utii mbele ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (watatu kulia), akiwa katika picha na Kamishna wa Utawala na Fedha, Michael Shija (wapili kulia), Kamishna wa Oparesheni Billy Mwakatage (kushoto) na Kamishna wa Usalama dhidi ya Moto, Jesuald Ikonko (kulia) wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Leave a comment  1