Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara

Uncategorized

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa Benki ya CRDB, walipotembelea Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Dar es Salaam. (Wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (wa kwanza kushoto) akizungumza na Kamishna wa Operesheni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (wa kwanza kulia) pamoja na maafisa wa Jeshi hilo, mikakati ya kudumisha uhusiano baina ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Benki ya CRDB, wakati wa kikao na Uongozi wa Benki ya CRDB, walipotembelea Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Dar es Salaam.

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Peter Mabusi, akifafanua jambo kwa Uongozi wa Benki ya CRDB, wakati wa kikao walipotembelea Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Dar es Salaam. (Wa kwanza kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei na (wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Operesheni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage.

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (watano kulia),  akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (mwenyesuti nyeusi), Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliombatana na Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo na Viongozi Waandamizi wa Benki ya CRDB, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye atembelewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Phaustine Kasike mapema leo asubuhi katika Makao Makuu ya Jeshi hilo, yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam. Lengo ni kujitambulisha na kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili vya Ulinzi na Usalama.

Katika ziara hiyo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, alitumia fursa hiyo kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza na kumuahidi ushirikiano katika kulijenga Taifa.

Vilevile Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike amepata fursa ya kujifunza jinsi gani Jeshi hilo linavyoendesha shughuli zake pamoja na kufanya mazungumzo ya kina na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo.

 “Nimejifunza mengi lakini pia nashukuru kwa kupata fursa ya kutembelea na kuona ni jinsi gani tunaweza kushirikiana” alisema Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike, baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kukuza mahusiano katika vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kukuza mahusiano katika vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, (Kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza wakati wa Kikao na Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Katikati ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye na kushoto ni Kamishna wa Usalama dhidi ya moto, Jesuald Ikonko. Kikao hicho kimefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ambaye alitembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam na kufanya kikao kilichowashirikisha Maofisa na Askari (hawapo pichani). Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Kamishna wa Operesheni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, akiwasilisha taarifa ya shughuli za Jeshi hilo mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kulia), wakati wa ziara ya waziri alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Kamishna wa Usalama dhidi ya moto, Jesuald Ikonko, akiwasilisha taarifa ya shughuli za Jeshi hilo mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), wakati wa ziara ya waziri alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani), wakati wa ziara ya waziri kutembelea Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (A/ISNP) Frank Meshack akionesha namna kifaa maalumu cha kung’amua moto kinavyofanya kazi (Smoke Detector) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ufungaji wa mifumo ya kugundua na kung’amua moto katika hatua ya awali mashuleni iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa International Labour Organization (ILO) jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Wakurugenzi wa Wilaya ya Kahama, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote wa jiji la Dar es Salaam, Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu pamoja na Makamanda wa Mikoa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ufungaji wa mifumo ya kugundua na kung’amua moto katika hatua ya awali mashuleni iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa International Labour Organization (ILO) jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Wakurugenzi wa Wilaya ya Kahama, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote wa jiji la Dar es Salaam, Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu pamoja na Makamanda wa Mikoa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dar es Salaam.

Sehemu ya Wakurugenzi wa Wilaya ya Kahama, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote wa jiji la Dar es Salaam, Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu, Makamanda wa Mikoa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia uwasilishwaji wa namna ya ufungaji wa mifumo ya kugundua na kung’amua moto katika hatua ya awali mashuleni. Hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa International Labour Organization (ILO) jijini Dar es Salaam, hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Wakurugenzi wa Wilaya ya Kahama, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote wa jiji la Dar es Salaam, Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu pamoja na Makamanda wa Mikoa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akitoa neno la shukurani kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama (mwenye suti), Wakurugenzi wa Wilaya ya Kahama, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote wa jiji la Dar es Salaam, Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu, Makamanda wa Mikoa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwa kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ufungaji wa mifumo ya kugundua na kung’amua moto katika hatua ya awali mashuleni iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa International Labour Organization (ILO) jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Leave a comment  1

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye wakati alipotembelea kituo cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala, Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokojia wakati alipotembelea kituo cha Jeshi hilo Mkoa wa ilala, jijini Dar es Salaam kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua baadhi ya vifaa, magari na mitambo inayotumiwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakati alipotembelea kituo cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Thobias Andengenye. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limepokea tuzo ya cheti cha heshima kwa kutambua mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji hapa nchini kutoka katika Taasisi ya Wazalendo na Maendeleo. Tuzo hiyo imepokelewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo Dar es salaam

Akizungumza Kamishna Jenerali baada ya kupokea tuzo ya cheti hicho. Alisema, anawashukuru Taasisi hiyo kwa kulipa Jeshi hilo tuzo hiyo kwa kazi nyingi ambazo taasisi hiyo imezifanya kwa kushirikia na Jeshi hilo ikiwepo kampeni ya kuitangaza namba ya simu ya dharura 114.

Kamishna Jenerali Andengenye, amezitaka Taasisi nyingine kushirikiana na Jeshi hilo katika kuzifufua Fire Hydrant zilizo haribika na zilizofukiwa ili kuongeza idadi ya vifaa hivyo ambayo ni msaada mkubwa wakati wa majanga ya moto. ‘‘Jamii ishirikiane na Jeshi letu katika kuvilinda visima hivyo (Fire Hydrant) vilivyopo mitaani kwani ni msaada mkubwa pale majanga ya moto yanapotokea’’.

Ni vema sasa mamlaka zinazoshughulikia miundombinu ya maji safi kwenye miji na majiji ikazingatia wanapotengeneza miundo mbinu hiyo, wakumbuke kuweka na mifumo ya maji ya zimamoto Fire Hydrant, pamoja na kuhakikisha wamiliki wanaojenga majengo makubwa na madogo wanaweka mifumo hiyo ya maji.

Tuna changamoto kubwa kwa upande wa visima hivyo, kwa hiyo kamapeni yetu ya kufufua na kuongeza visima hivyo vitasaidia kuleta tija katika utendaji kazi katika fani yetu. Tunashirikiana na Mamlaka za Maji kuhakikisha miundo mbinu hiyo inarudi na kutoa ushauri pale miradi mipya ya maji inapo jengwa.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania Muhammad Shaban alisema wamechukua uamuzi huo wa kutoa Tuzo hiyo kutokana na kuona mchango mkubwa wa Jeshi hilo walioutoa katika jamii. Pia amesema wataendea kutoa ushirikiano na Jeshi hilo katika utoaji elimu kwa umma. “Tupo tayari kushirikiana na Jeshi hili kuwaonesha sehemu zote ambazo fire hydrant zilizopo Mkoa wa Dar es salaam.”

“Kampeni ya kufufua fire hydrant imetugusa sana na kuona hatua hiyo ni msaada mkubwa kwa jamii kwani zitasaidia magari ya zimamoto na uokoaji kupata maji eneo la karibu majanga ya moto yanapotokea.”

Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Muhammad Shaban (wapili kulia) akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye tuzo ya cheti cha heshima, kwa mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akionesha zawadi ya fulana ya mabalozi wa Taasisi ya Salama Salimini aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Muhammad Shaban (kushoto), kama alama ya kutambua mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji, (kulia) ni balozi wa Salama Salimini Mwinyi Mangara. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa tuzo ya cheti cha heshima kutoka kwa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), kwa mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (wa tatu kulia) akiwa na Viongozi Waandamizi wa Jeshi pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Muhammad Shaban (wapili kushoto), (kulia) Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo Billy Mwakatage, (kushoto) Kamishna wa Usalama Dhidi ya moto Jesuald Ikonko na (wapili kulia) ni balozi wa Salama Salimini Mwinyi Mangara. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski akilakiwa na wenyeji wake alipo wasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam yaliyopo wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Balozi huyo ametembelea Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi.

Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski (kulia) akisaini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi. (kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye aliyeketi (mbele) akisoma taarifa ya Jeshi hilo kwa Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski (wa pili kulia) alipotembela Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski (wa pili kushoto), wengine ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CF) Billy Mwakatage (wa pili kulia), Kamishna wa Usalama Dhidi ya Moto, (CF) Jesuald Ikonko (wa kwanza kushoto) na msaaidizi wa Balozi wa Poland hapa nchini, Bi. Ewelina Lubieniecka (kulia).

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye (kushoto), akimsikiliza kwa makini msaaidizi wa Balozi wa Poland hapa nchini, Bi. Ewelina Lubieniecka (kulia) wakati wa mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi. (Wa pili kulia) ni Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski.

Picha ya pamoja.

(Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI