Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara

Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeungana na wanawake duniani kuadhimisha siku hiyo

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi alisema katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano (5) kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya, kupitia Jeshi hilo Nzalayaimisi aliwaongoza Askari (wanawake) kutembelea kituo cha Pedderef Sober House na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali.

Ambapo aliiomba jamii isiwanyanyapae pamoja na elimu wanayoendelea kuipata kituoni hapo ameiasa jamii kujitokeza kuwasaidia na kuwawezesha kwa hali na mali ili waweze kujiajili wenyewe kwani wanapotoka kituoni hapo wanakuwa hawana uwezo wakujiajili na kujikuta wanarudia tena kwenye janga la madawa hayo.

Pia Nzalayaimisi aliendelea kusema kwa kutoa pongezi kwa serikali na wadau mbalimbali wote waliojitokeza na kuthubutu kufanya maamuzi ya kujitoa katika kupambana na janga hilo na pia alimpongeza mkuu wa mkoa wa dar es salaam paul makonda kwa kuongoza mapambano hayo.

Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe naye alisema napenda kutoa shukrani za kipekee kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa msaada wao wa hali na mali waliotupatia na kuomba taasisi nyingi na wadau mbalimbali kujitokeza katika kusaidia kituo hiki kwani wengi wamenufaika kutokana na elimu na malezi wanayoendelea kuyapata kituoni hapo.

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi (kushoto) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa kituo  People With Drugs Dependence Relief Foundation (Pedderef),  Nuru Salehe wakati wa sherehe ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani mapema leo asubuhi. Kulia ni Jacqueline Samson na Ashura Diwani.

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi akitoa nasaa kwa wanawake na vijana walioathirika na janga la madawa ya kulevya kituoni hapo mapema leo asubuhi.

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi akimpa mkono wa pongezi mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe kwa jitihada anazoendelea kuzifanya katika kuhakikisha waathirika wote wa madawa ya kulevya waliopo kituoni kwake wanapata elimu ya kutosha na hatimaye kuacha kabisa utumiaji wa madawa hayo.

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jennifer Shirima ambaye aliambatana na msemaji wa Jeshi hilo katika ziara hiyo akiwasisistizia wanawake hao kutoajiingiza tena kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya na kuwakumbusha kuwa “Wanawake ni msingi wa mabadiliko kiuchumi” (kulia) ni Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe na (kushoto) ni Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi ambaye pia ni msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Moja ya wanawake waathirika wa madawa ya kulevya bi. Jacqueline Samson aliyesimama (katikati) akitoa shukrani kwa viongozi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambao hawapo picha kwa kuwatembelea kituoni hapo pia kwa msaada waliowapatia.

Maafisa na Askari (Wanawake) wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Mkurugenzi wa People With Drugs Dependence Relief Foundation (Pedderef) bi. Nuru Salehe wa kwanza mbele (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake waliopata kuathirika na madawa ya kulevya kituoni hapo, ambapo wanawake hao wameanza kurejea katika hali zao za kawaida mara baada ya kupewa elimu na malezi yanayostahili.

Viongozi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na Naibu Kamishna Jenerali wametembelea kiwanda cha kutengeneza magari na mitambo ya Jeshi hilo kilichopo Ruvu Mlandizi Mkoani Pwani.Naibu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Lidwino Mgumba kulia akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kiwanda kitakachotengeneza magari ya Zimamoto na Matrekta kilichopo eneo la Ruvu – Mlandizi Mkoani Pwani mapema leo asubuhi.  

 1Read more

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Puyo Nzalayaimisi (wapili kushoto) akizungumza na wazazi waliozaa watoto njiti kabla ya Jeshi kuwapa misaada mbalimbali kwa ajili ya kusaidia malezi ya watoto hao waliozaliwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke, jijini Dar es Salaam. Jeshi la Zimamoto lilianzimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani kwa kuitembelea hospitali hiyo ambapo walitoa zawadi mbalimbali kwa watoto njiti, watoto wanaoumwa na watoto waliozaliwa kwa njia ya operesheni. Wapili kulia(aliyebeba zawadi) ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi hilo, Maria Kulaya. Picha zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Dk. Ayoub Rioba akimkabizi kitabu cha wageni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye alipotembelea ofisi za Shirika hilo mikocheni mapema Agosti 5 2016.

 Kamishna Jenerali Thobias Andengenye (wa kwanza kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea ofisi za Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dk. Ayoub Rioba na wa pili ni Kaimu Kamishna wa Usalama dhidi ya moto Fikiri Salla .

 Mkurugenzi wa Matukio wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Bi Martha Swai (wa kwanza kulia) akitoa maelezo jinsi ya upokeaji wa habari za matukio mbalimbali kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (katikati) alipotembelea ofisi hizo mapema leo asubuhi (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Dk. Ayoub Rioba .

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  Thobias  Andengenye aliyesimama mbele, akimsomea taarifa ya Jeshi hilo Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Dk. Ayoub Rioba alipotembelea ofisi za Shirika hilo mapema.

 Kamishna Jenerali Thobias Andengenye (katikati) akipokea maelezo jinsi ya chumba cha matangazo kinavyofanya kazi (Studio) kutoka kwa Mtangazaji Bi Anna Mwasyoke hayupo pichani, (kushoto) ni Mkurugenzi mkuu wa TBC Taifa Dk. Ayoub Rioba.

Kaimu Kamishna wa Usalama dhidi ya moto Fikiri Salla (wa kwanza kushoto waliokaa) akitoa maelezo jinsi ya kutumia kizimia moto cha awali (Fire Extinguisher) iliopo kwenye gari la kurushia matangazo (OB Van) .

 2