Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage, akiwapa pole Waathirika wa moto ulioteketeza vibanda vya Wafanyabiashara wa Soko la Nguo Mbagala Temeke Jijini Dar es Salaam. Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi.

Kamaishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage akimfariji kwa kumpa pole Mama lishe Bi. Fatma Hassan aliyeunguliwa na vitendea kazi vyake kufuatia tukio la kuungua kwa moto kwa soko la nguo Mbagala.  Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi.

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage (kulia) akikagua eneo la Soko la Nguo Mbagala lililoteketea kwa moto juzi. Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi. (kushoto) ni Mwenyekiti Msaidizi wa Wafanyabiashara Harruni Kwemeye.

Sehemu ya Wafanyabiashara wa Soko la Nguo Mbagala Temeke Jijini Dar es Salaam walioathirika na moto ulioteketeza vibanda vya wafanyabiashara hao juzi. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini (CGF), Thobias Andengenye amewapandisha vyeo Askari wawili (2) wa Jeshi hilo kutokana na utendaji uliotukuka. Kamishna Jenerali amewapandisha vyeo kwa Mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa sheria.

CGF Thobias Andengenye, amefanya hivyo kutimiza Mamlaka hiyo ambayo ipo kwa mujibu wa sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Na. 14 ya mwaka 2007 na Kanuni ya Utumishi ya Jeshi hilo ya mwaka 2008.

Katika zoezi hilo amewapandisha vyeo Askari kutoka Konstebo wa Zimamoto kuwa Sajini wa Zimamoto, Askari waliopandishwa vyeo ni Konstebo Aloyce Zengwe ambaye alishiriki matembezi ya Skauti kwa kupeperusha bendera ya Jeshi hilo kutoka Morogoro mpaka Dodoma huku akihamasisha Wananchi kushirikiana na Jeshi hilo katika swala zima la Kuokoa Maisha na Mali.

Mwingine ni Konstebo Bahati Lugodisha aliyeshiriki Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017. Aidha Kamishna Jenerali aliwapa pongezi Askari waliopanda vyeo ambao hakika wanastahili na kuwataka watumie vyeo hivyo vipya kutimiza majukumu yao kwa weledi.

Akitangaza kupitia Force Order Na.FRF 09/2018 ya tarehe 02 March, 2018. Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji amewapongeza NCO hao kwa kupanda vyeo. “Hakika wanastahili na nawatakia utendaji mwema” alisema Kamisha Jenerali.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

 

 

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini (CGF), Thobias Andengenye amewapandisha vyeo askari 283 katika Mikoa yote Tanzania Bara. Kamishna Jenerali amewapandisha vyeo leo kwa Mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa sheria.

Kamishna Jenerali (CGF) Thobias Andengenye, amefanya hivyo kutimiza mamlaka hiyo ambayo ipo kwa mujibu wa sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Na. 14 ya 2007 na Kanuni ya Utumishi ya Jeshi hilo ya mwaka 2008.

Katika zoezi hilo amewapandisha vyeo Askari kutoka Sajini kuwa Stesheni Sajini 43, wengine 129 kutoka Koplo kuwa Sajini pamoja na 111 kutoka Konstebo kuwa Koplo na kuwataka Askari hao kufanya kazi kwa bidii.

“Mliopanda vyeo leo sio kwamba ninyi ni bora zaidi ya wengine bali ni kwa sababu ya bidii yenu kazini” alisema Kamishna Jenerali. Pia ni vema ambao hamjabahatika kupenda vyeo leo muongeze bidii katika utendaji kazi wenu.

Aidha Kamishna Jenerali aliwapa pongezi Askari waliopanda vyeo ambao hakika wanastahili na kuwataka watumie vyeo hivyo vipya kutimiza majukumu yao kwa weledi.

Naye Stesheni Sajini Ignas Uria amemshukuru Kamishna Jenerali na ameahidi kuongeza juhudi katika kukitumikia cheo hicho kwa weledi zaidi, huku akiwataka Askari wachini ya cheo chake na wajuu kushirikiana kwa pamoja katika kulitumikia Jeshi na Taifa kwa Ujumla.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Takwimu Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (ACF) Maria Kullaya amepokea msaada wa Kompyuta mpakato moja na Printa moja kutoka katika Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.Ltd, kwa ajili ya kuboresha kitengo cha Takwimu cha Jeshi hilo.

Msaada huo wenye thamani ya sh.1.5 million ambao umetolewa na Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.Ltd umepokelewa mapema leo Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliopo barabara ya Ohio Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati akipokea msaada huo Kamishna Msaidizi Maria alisema, msaada huu umetolewa wakati muafaka kwani utasaidia kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi katika ukusanyaji wa taarifa na utunzaji wa kumbukumbu tofauti na hapo awali.

Tunatarajia kuvitumia vifaa hivi kwa lengo mahususi pamoja na kuvitunza vizuri “Vifaa hivi vitakuwa chachu kwa kitengo cha takwimu kwani tulikuwa na uhaba wa vitendea kazi” alisema Kamishna Msaidizi Maria.

Naye Meneja wa Kampuni hiyo Bw. Rigobert Massawe, akizungumza wakati akikabidhi msaada huo, alisema “lengo ni kuliwezesha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutimiza majukumu yake kwa ufanisi kwani kwa kufanya hivyo tunatimiza wajibu wetu wa kurudisha huduma kwa jamii”.

Kamishna Msaidizi Maria anaishukuru kampuni hiyo kwa kuwapa msaada wa vitendea kazi hivyo, pia kupitia nafasi hii naomba wadau wengine waige mfano huu kwa kulisaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Nyanja mbalimbali ili liweze kutimiza majukumu yake ya kuokoa Maisha na Mali za Watanzania.

Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Takwimu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Msaidizi (ACF) Maria Kullaya (kulia) akipokea msaada wa Kompyuta mpakato na Printa kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.ltd Bw. Rigobert Massawe (kushoto). Vifaa vitakavyosaidia kutunza kumbukumbu za takwimu za majanga mbalimbali yanayotokea nchini, msaada huo umepokelewa Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo.

Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Takwimu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Msaidizi (ACF) Maria Kullaya wa nne kutoka (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.ltd Bw. Rigobert Massawe wa tano kutoka (kulia), Meneja rasilimali watu wa Kampuni hiyo Bw. Danial Mbonea wa tatu kutoka (kulia) na Maafisa wa Jeshi hilo wakati wa makabidhiano ya msaada wa Komputa mpakato na Printa, mapema leo Makao Makuu ya Jeshi hilo.

Meneja wa Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.ltd Bw. Rigobert Massawe (kushoto) akimkabidhi Kompyuta mpakato (Laptop) Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Takwimu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Msaidizi (ACF) Maria Kullaya (kulia) (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye katika picha ya pamoja na Kikosi cha Maokozi cha Jeshi hilo, wakati alipotembelea Kikosi hicho kilipokuwa kikionesha zoezi la maokozi, wa tatu kutoka (kulia) ni Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto Bashiri Madhehebi ambaye ni Mkuu wa kikosi hicho.

Wazamiaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakimuonesha Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo (hayupo pichani), jinsi wanavyoweza  kufanya maokozi katika maji alipotembelea eneo la daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni walipokuwa wakifanya zoezi hilo, mapema leo asubuhi (kushoto) ni Sajini wa Zimamoto Salehe Salla na aliyevaa boya maalum kwa ajili ya maokozi ni Koplo wa Zimamoto Omary Katonga.

Mzamiaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Sajini wa Zimamoto Saidi Sekibojo akiwa katika mazoezi ya uzamiaji katika eneo la Daraja la Mwalimu Nyerere mapema leo asubuhi, lengo ni kujiweka tayari kwa ajili ya Maokozi majini pindi ajali zinapotokea.

Sehemu ya Askari wazamiaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na Koplo Omary Katonga (kulia) wakionesha utimamu mbele ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo (hayupo picha) mara baada ya kufanikiwa kumuokoa mhanga aliyekuwa kazama katika kina kirefu cha maji, wakati wa mazoezi ya uzamiaji katika eneo la Daraja la Mwalimu Nyerere mapema leo asubuhi, lengo ni kujiweka tayari kwa ajili ya Maokozi majini pindi ajali zinapotokea. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akisalimiana na Balozi wa Cuba hapa nchini, Profesa Lucas Domingo Hernades Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo wa Cuba alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi tarehe 01/02/2018.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye aliyeketi (mbele) akisoma taarifa na changamoto zinazolikabili Jeshi hilo Balozi wa Cuba hapa nchini, Profesa Lucas Domingo Hernades Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo wa Cuba alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi tarehe 01/02/2018.

Balozi wa Cuba hapa nchini, Profesa Lucas Domingo Hernades akizungumza jambo wakati mazungumzo yao na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto), Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo hawapo pichani na Katibu wa Balozi na Mkalima, Sultan Hamud Said (Kulia) Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo wa Cuba alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi tarehe 01/02/2018.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akiwa katika picha na Balozi wa Cuba hapa nchini, Profesa Lucas Domingo Hernades Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam wengine ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Michael Shija wanne kutoka (kulia), Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage wa kwanza (kulia) na Kamishna wa Usalama Dhidi ya Moto, Jesuald Ikonko wa tano kutoka (kulia). Balozi huyo wa Cuba alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi tarehe 01/02/2018.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akiagana na Balozi wa Cuba hapa nchini, Profesa Lucas Domingo Hernades Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza mazungumzo yao mapema leo asubuhi tarehe 01/02/2018. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (katikati) akiongea na Waandishi wa habari wa radio Times Fm wakati akitoa taarifa ya Mafanikio ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ya mwaka 2017, kabla ya kukabidhiwa Tuzo na Cheti cha heshima kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kushoto) kwa kutambua utendaji kazi wa Jeshi hilo, Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kushoto) akitoa pongezi na shukrani kwa Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (katikati) wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo na cheti cha heshima kwa kutambua utendaji kazi wa jeshi hilo (kulia) ni Mkurugenzi wa vipindi Times Fm Bw. Amani Misana wakati wa Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.

Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (katikati) kwa kutambua utendaji kazi wa Jeshi hilo wakati wa Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.

Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko akipokea Tuzo ya heshima toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa kutokana na utendaji kazi wa Jeshi hilo kwa jamii na Taifa kwa ujumla (kulia) ni Mkurugenzi wa vipindi Times Fm Bw. Amani Misana wakati wa Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.

Picha ya Pamoja, Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (wa nne kulia) akiwa na Viongozi Waandamizi wa Jeshi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kulia kwake) na (kushoto kwake) ni Mkurugenzi wa vipindi Times Fm Bw. Amani Misana Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

 

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye kushoto akimkaribisha Kaimu Mkuu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela kulia alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 23/01/2018.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam, wakati alipofanya ziara yake mapema jana tarehe 23/01/2018.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (aliyeketi mbele) pamoja na Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo wakimfuatilia kwa karibu, Kaimu Mkurugenzi MKuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela, wakati wa mazungumzo yao alipotembelea  Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 23/01/2018.

Picha ya Pamoja, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (wa pili kushoto) akiwa na Viongozi Waandamizi wa Jeshi pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela (wa tatu kulia), mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo, Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 23/01/2018.(Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

                                         

                                             IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini limefanya Tamasha la utoaji elimu ya Kinga na Tahadhali dhidi ya majanga ya moto na majanga mengine katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo eneo la Kawe Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Majeshi na Kiserikali pamoja na Wananchi.

Tamasha hilo ambalo limeshirikisha wadau mbalimbali yakiwemo makampuni, taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali, shule za msingi na sekondari wanamichezo, wasanii, vyombo vya habari na wadau wengine.

Akizungumza wakati wa Tamasha hilo, Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, Billy Mwakatage alisema lengo kuu la tamasha hili ni kutoa elimu na kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya namba yetu ya dharura 114 inayotumika kutolea taarifa pindi wanapopatwa na majanga mbalimbali.

Kauli mbiu ya tamasha hili ni “Shiriki kukuza Uchumi wa Viwanda kwa kupunguza Majanga mbalimbali, piga simu 114”

Mwakatage alisema “niwatoe hofu wawekezaji wote wanaokuja kuwekeza hapa nchini kuwa, Jeshi letu limejipanga na linavifaa vya kisasa katika kukabiliana na majanga ya moto na majanga mengine kwa kuzingatia kauli mbiu ya Serikali kuwekeza kwenye viwanda”

Naye Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kanda Maalum ya Dar es Salaam Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto Peter Mabusi, amewataka Wanachi wa Jiji la Dar es Salaam kutembelea viwanja hivyo ili waweze kupata elimu na kuona ni jinsi gani Jeshi lao lilivyo na uwezo mkubwa wa kupambana na majanga mbalimbali.

Pia alisema “nawaomba Wananchi waweze kujitokeza kwa wingi viwanjani hapa kesho tarehe 23/12/2017 ambapo kutakuwa ni kilele cha Tamasha hili na litafungwa Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Eng. Hamad Masauni na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali”. Ufungaji wa tamasha hili utaambatana na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii pamoja na wanamichezo kama vile mpira wa pete, mpira wa miguu, kuvuta Kamba, kukimbiza kuku na michezo mingine.

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (Katikati), akizungusha king’ora kama ishara ya Uzinduzi rasmi wa Tamasha la Zimamoto la utoaji elimu kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Thobias Andengenye, wakati wa Tamasha la hilo lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo eneo la Kawe mapema jana asubuhi tarehe 22/12/2017. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, akizungumza na Wananchi wa Jiji la Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi rasmi wa Tamasha la Zimamoto la utoaji elimu kwa Umma, wakati wa Tamasha hilo lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo eneo la Kawe mapema mapema jana asubuhi tarehe 22/12/2017. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)