Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara

Blog Timeline Right Bar

Mkurugenzi wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Prof. Egird Mubofu (kulia), akizungumza na Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko, (kushoto) alipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo, wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko, akimkabidhi kipeperushi chenye namba ya dharura 114 ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkurugenzi wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Prof. Egird Mubofu (kulia), wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko, akielekea katika ukumbi wa Mikutano kwa mazungumzo, akiwa ameambatana na mwenyeji wake ambaye ni Afisa habari wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bi. Neema Mtema (wapili kulia), pamoja na Maafisa wa Jeshi mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Shirika hilo, wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko, akimuelezea majukumu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mwenyekiti wa Kikao Kaimu Mkuu wa Kitengo cha uhakiki (HCERT), Eng. Agnes Kiweru ambaye hayupo pichani, wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Mkurugenzi wa Viwango wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Bi. Edna Ndumbaro (katikati), akitoa ufafanuzi kwa hatua walizozichukua kuhusiana na vifaa vya Zimamoto, wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, (kulia) Kaimu Mkuu wa Kitengo cha uhakiki (HCERT), Eng. Agnes Kiweru, mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tanga, wakipambana na moto wa gari(Bus) mali ya Kampuni ya Tashriff Coach, mara baada ya kushika moto tukio lililotokea  eneo la Pongwe juzi mchana.(Picha kwa hisani ya mtandao)

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeundwa na kufanya kazi chini ya sheria namba 14 ya mwaka 2007 “FIRE AND RESCUE FORCE ACT”. Majukumu makubwa ya Jeshi ni kuzima moto na kuokoa maisha na mali katika majanga yatokanayo na moto, mafuriko, tetemeko la ardhi, ajali za barabarani pamoja na majanga mengineyo.

HUDUMA YA ZIMAMOTO NA UOKOAJI INATOLEWA.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeundwa kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa jamii. Hivyo basi mtu yoyote anastahili kupata huduma hiyo kwa kupiga namba ya simu 114. Pia kuna huduma nyingine zitolewazo na Jeshi.

HUDUMA ZITOLEWAZO NA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linajukumu kubwa la kutoa huduma kwa jamii katika Nyanja mbalimbali zikiwemo Kuokoa maisha ya watu na mali zao, Kuzima moto, Kutoa elimu ya kinga na tahadhari ya majanga moto, Kufanya ukaguzi wa tahadhari na kinga ya moto, Kusoma ramani za majengo na kutoa ushauri, Kutoa huduma ya kwanza katika majanga na ajali barabarani, Kutoa mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto, Kufanya uchunguzi kwenye majanga ya moto na Kutoa huduma za kibinadamu.

KUFIKA KWENYE TUKIO BILA YA VITENDEA KAZI (MAJI)

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wote huwa limejiandaa kwa magari yake kuwa na vitendea kazi vya kuzimia moto na kufanyia maokozi pia magari huwa yamejazwa maji wakati wote yanapokuwa vituoni yakisubiri matukio. Changamoto iliyopo ni wananchi wengi kuwa na imani kuwa magari ya Zimamoto huenda kwenye matukio bila maji.

AINA YA GARI LA ZIMAMOTO, VIFAA, UWEZO WA KUBEBA MAJI (UJAZO), NA JINSI YA UFANYAJI KAZI

Gari la Zimamoto linapofika kwenye tukio hufanya kazi kama mtambo wa kuzimamoto, magari hayo yanamatanki ya maji yenye ujazo kuanzia lita 1,500 hadi lita 7,000 (kuna moja linabeba lita 16,000) ili maji hayo yatoke kwa nguvu na kuweza kuzimamoto, magari ya Zimamoto yamefungwa pampu zenye uwezo wakusukuma lita 2,000 hadi lita 6,000 kwa dakika.

Kwa kawaida tunapofika kwenye tukio hutumia mipira yenye kipenyo cha milimeta 70 na kufunga kifaa cha kumwagia maji (branch pipe) chenye kipenyo cha milimeta 20 na pampu husukuma maji kwa nguvu ya bar 7, kwa vipimo hivyo huwa tunamwaga lita 1,000 kwa dakika kwa njia moja ya kutolea maji hivyo kwa gari lililobeba lita 7,000 maji yatakwisha ndani ya dakika saba, kwa kawaida tunatumia njia mbili za kutolea maji hivyo huwa tunamwaga lita 2,000 kwa dakika, na gari lililobeba lita 7,000 maji yatakwisha baada ya dakika 3½ nasisi hulazimika kuondoka eneo la tukio kwenda kutafuta maji.

Huku nyuma wanaweza kuja waandishi wa habari na kuwauliza wananchi mbona moto unawakana Zimamoto hawapo? Wananchi hujibu kuwa wamekuja lakini baada ya muda mfupi wameondoka na kusema kuwa wanakwenda kuchukua maji, hapo ndipo dhana ya Zimamoto wamekuja kuangalia kwanza ukubwa wa moto na sasa ndio wamekwenda kuchukua maji hujengeka. Ki uhalisia si kweli kuwa magari ya Zimamoto hufika kwenye tukio bila ya maji.

Maji yanayobebwa na magari ya Zimamoto husaidia kuanzia kazi, kabla maji ya kwenye gari kwisha gari la Zimamoto hutegemea kupata maji kutoka kwenye vituo maalum vya maji kwa ajili ya Zimamoto (Fire Hydrants) ambazo katika miji yetu mingi huwa hazifanyi kazi kutokana na sababu zifuatazo:-

Kutokuwa na maji

Kufukiwa na vifusi au mchanga au kufunikwa kutokana na ukarabati wa mitaa au barabara.

Kung’olewa na kubadilishwa matumizi.

Kung’olewa kwa alama za utambulisho (H sign)

Kuibiwa kwa mifuniko kutokana na biashara ya chuma cha kavu.

Miradi mingi ya maji katika miji kutoshirikisha ufungwaji wa vituo vya maji (Fire Hydrants).

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini – Thobias Andengenye anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna Mstaafu wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CF (OPS) Rogatius Peter Kipali, kilichotokea mapema leo Semptemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake Mombasa, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anatoa pole kwa Maafisa, Askari na Watumishi wote wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, familia ya Marehemu na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna tofauti tofauti.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na familia ya Marehemu linaendelea kuratibu shughuli za msiba huo na taarifa za Mazishi zitatolewa baadaye baada ya taratibu zote kukamilika.

 

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi

Amina.

 

 IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

 

Watu wengi wamekuwa wakikuta na kuvipita vifaa mithili ya mabomba ya kutoa maji pembezoni mwa barabara, maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu, viwanja vya ndege au viwanja vya michezo bila kufahamu vinafanya kazi gani.

Wengine hudhani ni mapambo ya barabara au alama Fulani kwenye maeneo hayo, ambapo baadhi yao hudiriki kuyatumia kinyume na kazi yake kutokana na kutotambua matumizi yake.

Mabomba haya (fire hydrants) sio mapambo bali ni mfumo uliounganishwa na mabomba makubwa ya maji, na kuwa visima vya maji ambapo gari la Zimamoto huchukua maji. Visima hivi vimejengwa makusudi kwa ajili ya kulirahisishia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea.

Mabomba hayo (Fire Hydrant) yana msukumo mkubwa wa maji na kusababisha maji yatoke kwa wingi na kwamuda mfupi. Uwepo wa vifaa hivyo sehemu mbalimbali za makazi ya watu na maeneo mengineyo hurahisisha zoezi zima la uzimaji moto, kwani pindi gari la kuzima moto linapoishiwa maji hujazwa hapohapo badala ya kuyafuata mbali na eneo la tukio.

Kwa kawaida magari ya zimamoto yana ujazo tofauti wa maji kuanzia lita 2000 hadi lita 16,000 ambapo ni ujazo mkubwa zaidi. Magari haya hubeba maji ya awali kwa ajili ya huduma ya kwanza ndio maana visima hivyo ni muhimu kuwepo.

Kwa nini tunasema ni maji kwa ajili ya huduma ya kwanza, ni kwa sababu ujazo wa maji yanayobebwa na gari la zimamoto ambao ni kati ya lita 2000 na lita 16000, hutoka kwamsukumo mkubwa, ambao kwa dakika moja maji yatatoka zaidi ya lita 1000 ukiwa unatumia mstari mmoja wa mpira wa maji (hose) na kusababisha maji hayo kuisha kwa muda mfupi.

Ukosefu wa visima hivyo sehemu mbalimbali, unapelekea Jeshi kushindwa kukabiliana na majanga ya moto kwa ufanisi baada ya maji yanayokuwa kwenye gari kuisha na kuwalazimu kwenda eneo la mbali.

Ingawa Jeshi la zimamoto na uokoaji linajitahidi kadri iwezekanavyo kuhakikisha linakabiliana vya kutosha na majanga ya moto kwa kusambaza visima hivi vya maji, lakini marakadhaa limekuwa linakumbana na changamoto mbalimbali hasa miundombinu.

Katika kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa, tayari baadhi ya Mikoa kama vile Dar es Salaam, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha na Tanga imejitahidi kuhakikisha miundombinu yake inakidhi kuruhusu ujenzi wa visima vya maji ya kuzimia moto na utaratibu umeandaliwa kuhakikisha mikoa Mingine inaboresha miundombinu yake kwa kuzingatia ujenzi wa huduma hiyo.

Pamoja na changamoto hizo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji bado linatekeleza wajibu wake kwa kuwa elimisha wananchi namna ya kutunza miundombinu hiyo na kusambaza mifumo hiyo kwa kiwango kinacho hitajika.

Wito kwa wananchi tuyatunze mabomba hayo (fire hydrant) kutokana na kuwa na umuhimu katika kurahisisha shughuli za kupambana na majanga ya moto, kwani kumekuwa na wimbi kubwa la uuzaji wa vyuma chakavu.

 

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI