Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara

Blog Timeline Right Bar

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye wakati alipotembelea kituo cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala, Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askari wa Jeshi la mersin escort kayseri escort adana escort istanbul nakliyat Zimamoto na Uokojia wakati alipotembelea kituo cha Jeshi hilo Mkoa wa ilala, jijini Dar es Salaam kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua baadhi ya vifaa, magari na mitambo inayotumiwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakati alipotembelea kituo cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Kushoto adana escort adana escort
kwake ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Thobias Andengenye. 
(Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limepokea tuzo ya cheti cha heshima kwa kutambua mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji hapa nchini kutoka katika Taasisi ya Wazalendo na Maendeleo. Tuzo hiyo imepokelewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo Dar es salaam

Akizungumza Kamishna Jenerali baada ya kupokea tuzo ya cheti hicho. Alisema, anawashukuru Taasisi hiyo kwa kulipa Jeshi hilo tuzo hiyo kwa kazi nyingi ambazo taasisi hiyo imezifanya kwa kushirikia na Jeshi hilo ikiwepo kampeni ya kuitangaza namba ya simu ya dharura 114.

Kamishna Jenerali Andengenye, amezitaka Taasisi nyingine kushirikiana na Jeshi hilo katika kuzifufua Fire Hydrant zilizo haribika na zilizofukiwa ili kuongeza idadi ya vifaa hivyo ambayo ni msaada mkubwa wakati wa majanga ya moto. ‘‘Jamii ishirikiane na Jeshi letu katika kuvilinda visima hivyo (Fire Hydrant) vilivyopo mitaani kwani ni msaada mkubwa pale majanga ya moto yanapotokea’’.

Ni vema sasa mamlaka zinazoshughulikia miundombinu ya maji safi kwenye miji na majiji ikazingatia wanapotengeneza miundo mbinu hiyo, wakumbuke kuweka na mifumo ya maji ya zimamoto Fire Hydrant, pamoja na kuhakikisha wamiliki wanaojenga majengo makubwa na madogo wanaweka mifumo hiyo ya maji.

Tuna changamoto kubwa kwa upande wa visima hivyo, kwa hiyo kamapeni yetu ya kufufua na kuongeza visima hivyo vitasaidia kuleta tija katika utendaji kazi katika fani yetu. Tunashirikiana na Mamlaka za Maji kuhakikisha miundo mbinu hiyo inarudi na kutoa ushauri pale miradi mipya ya maji inapo jengwa.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania Muhammad Shaban alisema wamechukua uamuzi huo wa kutoa Tuzo hiyo kutokana na kuona mchango mkubwa wa Jeshi hilo walioutoa katika jamii. Pia amesema wataendea kutoa ushirikiano na Jeshi hilo katika utoaji elimu kwa umma. “Tupo tayari kushirikiana na Jeshi hili kuwaonesha sehemu zote ambazo fire hydrant zilizopo Mkoa wa Dar es salaam.”

“Kampeni ya kufufua fire hydrant imetugusa sana na kuona hatua hiyo ni msaada mkubwa kwa jamii kwani zitasaidia magari ya zimamoto na uokoaji kupata maji eneo la karibu majanga ya moto yanapotokea.”

Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Muhammad Shaban (wapili kulia) akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye tuzo ya cheti cha heshima, kwa mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akionesha zawadi ya fulana ya mabalozi wa Taasisi ya Salama Salimini aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Muhammad Shaban (kushoto), kama alama ya kutambua mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji, (kulia) ni balozi wa Salama Salimini Mwinyi Mangara. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa tuzo ya cheti cha heshima kutoka kwa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), kwa mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (wa tatu kulia) akiwa na Viongozi Waandamizi wa Jeshi pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Muhammad Shaban (wapili kushoto), (kulia) Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo Billy Mwakatage, (kushoto) Kamishna wa Usalama Dhidi ya moto Jesuald Ikonko na (wapili kulia) ni balozi wa Salama Salimini Mwinyi Mangara. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski akilakiwa na wenyeji wake alipo wasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam yaliyopo wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Balozi huyo ametembelea Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi.

Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski (kulia) akisaini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi. (kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye aliyeketi (mbele) akisoma taarifa ya Jeshi hilo kwa Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski (wa pili kulia) alipotembela Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski (wa pili kushoto), wengine ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CF) Billy Mwakatage (wa pili kulia), Kamishna wa Usalama Dhidi ya Moto, (CF) Jesuald Ikonko (wa kwanza kushoto) na msaaidizi wa Balozi wa Poland hapa nchini, Bi. bedava bonus adana escort mersin escort canlı casino oyna bedava casino bedava bonus deneme bonusu bedava bonus veren bahis siteleri Ewelina Lubieniecka (kulia).

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye (kushoto), akimsikiliza kwa makini msaaidizi wa Balozi wa Poland hapa nchini, Bi. Ewelina Lubieniecka (kulia) wakati wa mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi. (Wa pili kulia) ni Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski.

Picha ya pamoja.

(Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi (INSP) Joseph Mwasabeja (kulia) akisalimiana na Meneja wa Kampuni ya Global Group Bw. Abdallah Mrisho (kushoto) alipotembelea Kampuni hiyo mapema leo.

Mwandishi na Mhariri wa gazeti la amani wa Kampuni ya Global Group Bw. Erick Evalist (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi (INSP) Joseph Mwasabeja (wa pili kulia), jinsi Kampuni ya Global Group inavyoendesha shughuli zake kupitia vyombo mbalimbali vilivyopo chini ya kampuni hiyo wakati wa ziara yake yakukuza mahusiano mapema leo.

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja (INSP) (wa pili kulia) akimsikiliza kwa makini mmoja ya watayarishaji wa vipindi wa Kampuni ya Global Group (aliyevaa shati ya blue) wakati wa ziara yake yakukuza mahusiano  alipo tembelea kampuni hiyo mapema leo. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage (kushoto), akiwa ameambatana na mwenyeji wake mmiliki wa Yatch Club Bw. Brian Fernandes (kulia), baada ya kuwasili ofisi za Yatch Club kwa ajili ya uzinduzi wa mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi.

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage (wa pili kushoto), akiwa na wakufunzi kutoka nchini Ujerumani na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Wakati wa  uzinduzi wa mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam. Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi.

Mkufunzi kutoka nchini Ujerumani Bw. Dan Jungingfer (kulia), akitoa maelekezo ya mbinu za uzamiaji majini kwenye kina kirefu kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Sajini Gift Longwe na Konstebo Baltazari Swai. Wakati wa  uzinduzi wa mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

Mafunzo haya yanayoendeshwa hapa nchini na Wakufunzi kutoka Ujerumani yana lengo la kuwaongezea Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji weledi katika kukabiliana na majanga ya mafuriko na kuzama kwa watu majini haswa kwenye kina kirefu.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Picha ni sehemu ya bweni lililoathirika na moto na kuteketeza mali za Wanafunzi. (Picha na Maktaba)

Jeshi la  Zimamoto na Uokoaji ndicho chombo chenye jukumu la kuzuia na kukabiliana na majanga  mbalimbali   kama mafuriko , Tetemeko la  Ardhi,  ajali  za vyombo vya usafiri na usafirishaji,  kuporomoka kwa majengo, migodi,  pamoja na matukio ya moto. 

Mara kwa mara, majanga ya moto yamekuwa yakitokea katika jamii yetu kwa sababu moto ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku.  Utafiti umethibitisha  kwamba,  vyanzo vingi vya moto ni sisi wenyewe (binadamu)  kutokana na uzembe,   hujuma  au kutokukuwa na  elimu ya Tahadhali na Kinga  Dhidi ya  Moto.

Aidha, matukio ya moto yamekuwa  yakitokea mara kwa mara katika shule za bweni hapa nchini  hususani shule za sekondari,  na kusababisha  uharibifu wa miundo mbinu kama vile Mali, majengo na wakati mwingine majeraha au vifo kwa wanafunzi wetu na kuleta simanzi na sintofahamu kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla .

Uchunguzi  wa moto (Fire Investigation)  umebaini     sababu  za matukio hayo ni matumizi mabaya ya umeme yanayofanywa na   wanafunzi  kwa  kujiunganishia nyaya za umeme wenyewe bila kuwa na weledi iliwapate  sehemu za kuchaji simu na heater za kuchemshia maji kwa kificho kwa sababu Wanafunzi  hawaruhusiwi kuwa na simu wala heater pindi wanapokuwa shuleni.

Lakini pia sababu nyingine ni matumizi ya mishumaa, unapokatika umeme wakati wa kujisomea. Shule nyingi  zinajaribu kuzuia mabweni kutumika kama sehemu za kujisomea,  lakini  bado wapo baadhi ya Wanafunzi  wanaamua   kujisomea  ndani ya  mabweni  bila kuchukua  tahadhari yoyote na wanapopitiwa na usingizi,  uacha mishumaa inaendelea kuwaka na hatimaye kusababisha ajali ya moto.

Utakumbuka miaka kadhaa iliyopita matukio kama haya ya kuungua kwa shule yalileta majonzi  makubwa kwa kuangamiza  maisha ya Wanafunzi wengi.  Kuungua kwa shule ya Shauritanga Mkoani Kilimanjaro mwaka 1994 ambapo zaidi ya wanafunzi 40 walipoteza Maisha pamoja na Mali.

Mwaka 2009 shule ya sekondari Idodi Mkoani Iringa iliteketea kwa moto na zaidi ya wanafunzi 20 walipoteza Maisha pamoja na Mali. Hiyo ni mifano tu lakini matukio ya kuungua kwa shule ni mengi sana hapa nchini.

Ili kupunguza matukio hayo, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeanzisha Fire klabu  katika shule mbalimbali  za Msingi na Sekondari ili kupata wajumbe  watakaoliwakilisha  katika shule na makazi yao.

Kwa kutumia fire klabu, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  limejenga ukaribu mkubwa na Wanafunzi wa shule hizo,  hatua inayosaidia kuwapa elimu stahiki ya kukabiliana na majanga ya moto.

Changamoto  iliyopo ni  mapokeo ya baadhi ya Viongozi wa shule kutokuwa tayari kuruhusu shule zao kuanzisha  klabu za Zimamoto zinazosimamiwa na  kuratibiwa na Jeshi hilo ambapo mpaka sasa ni shule 100 ndizo zilizofungua klabu hizo kwa nchi nzima.

Kama nilivyo eleza hapo mwanzo, lengo la klabu hizo ni kuwapa fursa wanafunzi kuwa familia moja na wataalamu wa Zimamoto. Ukaribu huo hutumika kwa wazimamoto kuwapa mbinu mbalimbali za kuzuia na kukabiliana na vyanzo vya moto.

Lakini  kwa upande wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,  ni kupanua wigo wa kuwa na idadi kubwa ya  watu, wanaoifahamu vyema  elimu  hiyo  na kuwa  mabalozi  wazuri  watakao liunganisha Jeshi  na jamii kwa kufikisha  elimu hiyo, Mijini  na Vijijini na hatimaye kuweza kupunguza na kutokomeza kabisa majanga.

Wito wangu kwa wamiliki wa shule, walipokee jambo hili kama ukombozi kwao kupunguza majanga  ya moto katika shule zao.

Tukishirikiana tutapunguza majanga ya moto, na Taifa litakuwa salama.

Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI