Jukumu la Jeshi kutoa huduma ya maokozi nchi kavu, majini na angani. Jukumu hili hutekelezwa kwa njia tofauti ikiwemo kuandaa mikakati ya maokozi iwapo dharura itatokea kwa kusudi la kupunguza idadi ya vifo pindi yatokeapo mafuriko, ajali za barabarani, tetemeko la ardhi. Kutoa ushauri kwa Serikali pamoja na Mashirika binafsi juu ya huduma ya maokozi. Huduma hizo hutoolewa pia bandari pamoja na viwanja vya ndege.